test

Alhamisi, 4 Agosti 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi siku ya Vijana Kitaifa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Mhe Mavunde alibainisha kuwa Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.

Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo Mhe. Mavunde alisema lengo la kauli mbiu hii ni kuzihimiza nchi wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana katika shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 2030.

Akizungumzia maadhimisho hayo Kitaifa Mhe . Mavunde alisema kuwa vijana watapata fursa ya kushiriki shughuli mbalimbali kama makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho ya Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.

“Tanzania tutasherekea siku ya Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii itaenda sambamba na Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.

Wazo la kuwa na siku ya Vijana Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka 1991 Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx