test

Ijumaa, 26 Agosti 2016

MWANAMKE ALIYECHOMA NYUMBA YA FAMILIA YAKE AJINYONGA MAHABUSU


MAHABUSU Victoria Edward (51) aliyekuwa anatuhumiwa kwa kosa la kuchoma nyumba yao ya familia, amejinyonga hadi kufa ndani ya chumba cha mahabusu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo wakati akizungumza na gazeti hili, alikiri kutokea kwa tukio hilo katika Kituo cha Kikuu cha Polisi saa 6:20 usiku jana wakati wenzake wakiwa wamelala.
“Polisi wa zamu alisikia kelele kutoka kwenye chumba cha mahabusu wa kike ambapo polisi walijitahidi kuokoa maisha ya mahabusu huyo, lakini ilishindikanika,” alisema Kamanda Mkumbo.
Mahabusu huyo, ambaye ni mkazi wa Lemara jijini hapa, alijinyonga kwa kutumia shuka lake alilokuwa anatumia kujifunikia wakati yuko mahabusi. Mtuhumiwa huyo, alijinyonga kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yake.
“Jana ilikuwa afikishwe mahakamani kujibu kosa lililokuwa linamkabili,” alisema Kamanda Mkumbo na kuwahakikishia kuwa hali ya usalama kituoni hapo na tukio hilo, havihusiani na sababu zozote za kiusalama.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx