test

Alhamisi, 25 Agosti 2016

MSIMU MPYA LIGI KUU YA VODACOM 2016/2017 WAANZA KWA MSISIMKO.




 Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara VPL ilifunguliwa rasmi wikiendiiliyopita kwa mechi 6 kuchezwa katika viwanja tofauti. Katika mechi ya Simba dhidiya Ndanda FC tulishuhudia Simba ikipata ushindi wa magoli 3 – 1 huku winga mpya wa Simba, Shiza Kichuya akifanikiwa kufunga bao zuri kuhitimisha karamu yamagoli 3.




 Kule Morogoro, Mtibwa Sugar wakiwa uwanja wa nyumba ni waliduwazwa na Ruvu Shooting baada ya kupokea kichapo cha goli moja bila. Akizungumza siku moja baada ya mechi hiyo Kocha wa Mtibwa Sugar Salum Mayanga alisema kipigo hicho kimewazindua usingizi ni hivyo wanajipanga zaidi kwa mechi zijazo.

Azam FC ilinusurika kupokea kipigo kutoka kwa African Lyon ambapo John Bocoo aliisawazishia timu hiyo katika dakika za majeruhi. Katika mchezo huo African Lyon walionekana kucheza kandanda safi, “hii timu inacheza kana kwamba ilikuwa inacheza ligi kuu kwa muda mrefu sana, itasumbua kweli kweli” alisikika mmoja wa watazamaji akifuatilia mechi hiyo kupitia “KibandaUmiza” maeneo ya Kijitonyama. Nae kocha mkuu wa klabu ya Azam FC ambayo mwaka huu imefanikiwa kuchukua Ngao ya Jamii alisema kuwa anahitaji muda zaidi ili kukisuka kikosi chake na kucheza kupitia mifumo wanayoendelea kuwafundisha wachezaji wa timu hiyo. “Kwa sasa tunafanya tathmini ya mchezo uliopita, kutoa makosa na kurekebishana pale tulipokosea, tukimaliza hapo kwa wiki hii tutaanza kujipanga kwa mchezo ujao (Majimaji), lakini cha kwanza tunaangalia yaliyaliyo tokea katika mchezo wa kwanza, mapungufu yalikuwa wapi na nani anapaswa kufanya nini,” alisema.

Mechiya Stand United naMbao FC timu iliyopanda daraja haikufanikiwa kutoa mshindi na kule Songea timu ya Majimaji ilikubali kupokea kichapo cha goli 1 – 0 kutoka kwa Tanzania Prisons. Hii leo kutakuwa na mchezo mmoja utakaochezwa jijini Mwanza ambapo Toto Africans itamenyanana Mwadui FC. Msimu uliopita mechi mbili za ugenini na nyumbani za timu hizi ziliisha kwa ushindi wa goli 1 bila huku kila timu ikitamba kwenye uwanja wake.  
Kwenye picha baadhi ya wafanyakazi kutoka Idara ya Masoko ya Vodacom Tanzania wakiongozwana Mkuuwa Idara hiyo Nandi Mwiyombella (katikati) walifika kushuhudia mechi kati ya  Simba na Ndanda.

Vinara wa LigiKuu ya Vodacom msimu uliopita hawakucheza mechi yao ya ufanguzi ilikupata nafasi ya kujiandaa na mechi ya Shirikisho dhidi ya TP Mazembe. Yanga itaanza kampeni ya msimu huu hapo Jumamosi kwa kucheza na African Lyon.


Endelea Kufuata kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii ukitumia  # VPL 2016 uweze kutabiri matokeo ya mechi na kupata taarifa zaidi kuhusu ligi kuu ya Vodacom. Pia kupata live match updates kila wiki.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx