WAZIRI Mkuu wa zamani aliyegombea urais kupitia Chadema na kuungwa mkono na mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Edward Lowassa, amesema Jeshi la Polisi linatumika vibaya.
Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwataka wananchi kuwa watulivu na wasifanye fujo baada ya zuio hilo la polisi.
“Wananchi endeleeni kuwa watulivu, polisi wamezuia mkutano halali, msifanye fujo yoyote na pokeeni maelekezo kwa viongozi.
“Niseme Jeshi la Polisi linatumika vibaya, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuivunja demokrasia ya vyama vingi na sheria na 5 ya mwaka 1992 ya uanzishwaji wa vyama vingi,” alisema Lowassa.