Aidha, kwa kuwa CUF inadai kwamba haiitambui serikali hiyo basi ruzuku kwa chama hicho isitishwe kuanzia sasa hadi hapo chama hicho kitakapoitambua rasmi serikali hiyo na kuacha kuhamasisha wananchi wasilipe kodi.
Katika barua ya chama hicho iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Augustine Mrema ilisema chama hicho kimesikitishwa na wanalaani kitendo kilichofanywa Hamad ambaye pia alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa wa Zanzibar (SUK) wakati wa maziko ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, marehemu Mzee Aboud Jumbe cha kukataa kumpa Rais Shein mkono wa kusalimiana.
Alisema kuleta tofauti za kisiasa msibani kwa makusudi, Maalim Seif ameendelea kuwagawa Wazanzibari kisiasa na kushindwa kumuenzi marehemu Aboud Jumbe, ambaye pamoja na kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu pia ndiye aliyemlea Maalim Seif kisiasa.
Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa marudio uliosusiwa na CUF, Maalim Seif amekuwa akileta chokochoko na uchochezi dhidi ya serikali ya Zanzibar akidai kwamba haitambui na kuwataka wananchi wa Zanzibar kugoma na kuwataka wasilipe kodi kwa serikali