Mkuu huyo wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka.
Kikao cha Kamati ya Maadili ya TFF, kilikaa bila ya Muro kuwepo kwa kuwa wakati mwaliko unatoka alikuwa nje ya Dar es Salaam.
Katika makosa matatu aliyoshitakiwa, moja amekumbana na adhabu hiyo, moja amepigwa faini ya Sh milioni 3 na moja ameonekana hana hatia.
Muro ambaye yupo mapumzikoni Machame mkoani Kilimanjaro ambako ni kwao.

