test

Jumatatu, 5 Oktoba 2015

Dr. Slaa Kurusha Makombora ya Mwisho Kwa LOWASSA.......Yadaiwa Atatumia Majukwaa ya ACT-Wazalendo Kuwaponda Viongozi wa UKAWA. USIKOSE




Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa anatarajiwa kurusha makombora yake ya mwisho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu dhidi mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa anayeungwa mkono na Ukawa. 
 
Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa Dk. Slaa ambaye ameonekana kuwa nchini wiki iliyopita baada ya kukaa ughaibuni kwa muda tangu alipomvaa Lowassa na Chadema, atapanda katika jukwaa la ACT-Wazalendo kwa lengo la kuyasema yake ya moyoni.

Watu  wa  karibu  na  Dr. Slaa  wamelieleza  gazeti  moja  kubwa  nchini  kuwa  mwanasiasa  huyo  mkongwe  amekubaliana  na  viongozi  wa  ACT-Wazalendo  na  atapanda  kwa  mara  ya  kwanza  katika  jukwaa  la  kampeni  la  chama  hicho  jumatano ( tarehe 7)  kumnadi  mgombea  ubunge  wa  chama  hicho  katika  jimbo  la  Iringa  Mjini,Chiku Abwao.

Taarifa  zaidi  zinaeleza  kuwa,Dr. Slaa  ataendelea  kuzunguka  katika  majukwaa  ya  kampeni  za  chama  hicho  huku  akitarajiwa  kuilipua  Chadema  na UKAWA  kwa  ujumla  kwa  tuhuma  zinazodaiwa  kuwa  ni  kupokea  pesa  kutoka  kwa  baadhi  ya  makada  wa  CCM  ili  kuwakubalia  kujiunga  na  chama  hicho.

Aidha,Dr  Slaa  atajiunga  na  Zitto  Kabwe  ambaye  alikuwa  ni  Naibu  Katibu  Mkuu  wake  wakati  wakiwa Chadema    na  kutofautiana  na  hivyo  Chama  hicho  kumfukuza  uanachama  chini  ya  uratibu  wa  Dr  Slaa  mwenyewe. 

Dr  Slaa  alitangaza  kujiuvua  uanachama  wake  Chadema  na  kustaafu  siasa  baada  ya  chama  hicho  kumpokea  na  kumpitisha  kuwa  mgombea  urais, Waziri  mkuu  wa  zamani, Edward  Lowassa.

Baada  ya  kustaafu  siasa,Dr  Slaa  alitoweka  hadharani  tangu  July  28  mwaka  huu  hadi  alipoibuka  mwanzoni  mwa  Septemba  katika  Hoteli  ya  Serena,Dar  es  Salaam  alipofanya  mkutano  na  waandishi  wa  habari  na  kutangaza  kujiuzulu.

Baada  ya  mkutano  huo  ambao  hata  hivyo  uliibua  maswali  mengi,Dr Slaa  alisafiri  na  familia  yake  kwenda  nchini Marekani  hadi  hivi  karibuni  aliporejea  nchini

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni