Baraza Kuu la Waislam Tanzania BAKWATA kwa kushirikiana na Serikali
kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, linafuatilia
tukio la kufariki dunia kwa mahujaji 107 katika Mji wa Makkah nchini
Saudia Arabia baada kuangukiwa na Mashine ya ujenzi ya kubeba vitu
vizito iliyosababishwa na Upepo mkali na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ali akizungumza na
waandishi wa habari amesema Mpaka sasa bado haijafahamika kama kuna
mahujaji kutoka Tanzania ambao wamefariki au wamepata madhara kutokana
na tukio hilo na kutaka waislamu kuwa watulivu huku bakwata wakifuatilia
ili kufahamu hatma ya mahujaji wa Tanzania walioko makkah.
Aidha kufuatia tukio hilo Mufti amewataka Maimamu wa Misikiti pamoja na
waislam wote nchini kuwaombea dua maalum mahujaji walifariki katika
ajali hiyo pamoja na majeruhi ili m/mungu awape nafuu na kuendelea na
ibada ya hija ikiwa ni utekelezaji wa nguzo ya tano ya Uislam.
Kuhusu idadi ya watanzania walioko katika ibada hiyo ya hija Mufti
amesema mpaka sasa bado bakwata haina idai kamiliki kwa kuwa bado
mahujaji kutoka Tanzania wanaelekea nchini Saudi arabia kwa ajili ya
hijja.
0 comments:
Chapisha Maoni