Mgombea
mwenza wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha
demokrasia na maendeleo (Chadema), chini ya umoja wa katiba ya wananchi (
UKAWA )Mh. Juma Duni Haji amesema kwamba iwapo Mh. Edward Lowassa
atachaguliwa na wananchi kuongoza serikali ya awamu ya tano atahakikisha
baadhi ya kodi pamoja na ushuru wa mazao wanaotozwa wakulima unafutwa
mara moja sambamba na kupiga marufuku mtindo wa serikali wa kuwakopa
wakulima mazao yao.
Mh. Duni ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa
kampeni za uchaguzi mkuu za kumnadi mgombea urais wa Chadema kupitia
UKAWA Mh. Edward Ngoyai Lowassa zilizofanyika katika mji mdogo wa maguu
jimbo la mbinga vijijini na katika jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma kwa
nyakati tofauti kufuatia malalamiko ya wakulima wa kijiji cha maguu
kukopwa kahawa yao yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12 msimu
wa 2014/2015.
Na je, ilani ya uchaguzi ya Chadema na UKAWA kwa ujumla imesema nini kuhusu elimu kwa mtoto wa kitanzania.
Katibu wa jumuiya ya wanawake wa chama cha wananchi (CUF ) taifa,
Fatuma Kalembo na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mkanyageni kisiwani Pemba
Mohammed Habibu Mnyaa ambao wanaongozana na mgombea mwenza wa urais Mh.
Juma Duni Haji wamezungumzia changamoto zinazowakabili wakulima wa
kahawa na mahindi wilayani Mbinga na namna ya kuziepa.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kampeni za mgombea
mwenza wa Chadema wamepata fursa ya kueleza kero zinazowakabili ndani ya
jimbo hilo la Mbinga vijijini.
0 comments:
Chapisha Maoni