Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo
cha aliyekuwa mmoja wa magwiji wa Tasnia ya Utangazaji hapa nchini Mzee
Godfrey Mngodo ambaye alifariki dunia, Ijumaa, Septemba 11, 2015 mjini
Dar es Salaam.
Katika salamu zake za rambirambi kwa Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, Rais Kikwete amesema
amesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee Mngodo ambaye amemweleza kama
kielelezo thabiti cha weledi na ubora wa Tasnia ya Utangazaji katika
Tanzania.
0 comments:
Chapisha Maoni