Wakazi wa Kigamboni hususan wanaotumia kivuko kwa usafiri wa magari
binafsi leo wamejikuta katika adha ya kukaa foleni kwa muda mrefu
kutokana na kutumika kwa kivuko kimoja cha Mv.Kigamboni ambacho kilikuwa
kikibeba magari yasiozidi sita kwa kila safari ya kwenda na kurudi.
Kutumika kwa kivuko kimoja kunatokana na kuharibika kwa kivuko kikubwa
cha Mv.Magogoni ambacho kinadaiwa kuharibika kuanzia saa sita mchana na
kuegeshwa pembeni kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo.
0 comments:
Chapisha Maoni