test

Jumapili, 13 Septemba 2015

Maalim SEIF asema hana mpango wa kuvunja serikali ya umoja wa kitaifa



Mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharrif Hamad amesema hana mpango wa kuvunja serikali ya umoja wa kitaifa
Mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharrif Hamad
Mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi  CUF Maalim Seif Sharrif Hamad  amesema  hana mpango wa kuvunja  serikali ya umoja wa kitaifa bali endapo atashinda kuwa  Rais wa Zanzibar atahakikisha anaimarisha muundo mzima wa serikali hiyo ili uweze kutoa fursa sawa kwa viongozi wote wa serikali
Amesema kuwa Chama cha Wananchi CUF ni muumini mkubwa wa kuimarisha amani ya Zanzibar tangu mnamo mwaka 1995 ambapo suala la amani limekuwa ni hoja ya msingi ya kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar.
Hata hivyo amesema katika serikali hiyo atahakikisha  mipango ya utekelezaji inapangwa kwa kuzingatia usawa wa vyama vyote ili kila chama kiweze kupata fursa ya kuchangia katika maendeleo ya nchi.


Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni