Mgombea urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataunda serikali itakayokuwa na viongozi wenye uwezo wa kuchukua hatua na kutatua matatizo ya wananchi na atahakikisha utaratibu wa wananchi kulalamika na viongozi pia kulalamika kama ilivyo sasa unabaki kuwa historia.
Mh
Lowassa ambaye amefanya mikutano minne katika majimbo ya Mtera, Bahi
Chilonwa na Dodoma mjini pia amewaomba watanzania kumpa nafasi ya
kukamilisha ndoto yake ya kuleta usawa wa huduma zakijamii ikiwemo elimu
aliyoanza kuonyesha mfano kupitia shule za kata alipokuwa waziri mkuu.
Nao
Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mh Fredrick Sumaye na mwanasheria
wa Chadema Mh Tundu Lisu wakihutubia jana mjini Dodoma walisema
kukithiri kwa malalamiko ya wananchi kukosa huduma huku wanaotakiwa
kuchukua hatua wakiendelea kutoa ahadi inatosha kuonyesha kuwa uwezo wao
wa kupata ufumbuzi umefika mwisho na ndio maana UKAWA inaomba nafasi ya
kuondoa tatizo hilo.
Wananchi
na viongozi wa jimbo la Mtera walisema ubinafisi wa viongozi wa CCM, na
ahadi zisizotekelezeka umesababisha wapoteze matumaini ya kuondokana na
umaskini hasa kwa vijana.
Akihitimisha
mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Dodoma uliofanyika jana Dodoma
mjini, Mh Lowaasa ambaye sasa anaelekea mkoa wa singida aliendelea
kunadi sera za UKAWA na kutoa ufafanuzi wa namna ya kuzitekeleza kwa
wakati na kwakasi inayostahili.
0 comments:
Chapisha Maoni