test

Jumamosi, 12 Septemba 2015

Walimu wacharazwa viboka huko Kimba kisa hiki hapa:



Walimu watatu wa kike wa shule ya Msingi Mwabagole wilayani Kwimba mkoani Mwanza wamevamiwa, kushambuliwa na kupigwa viboko na baadhi ya wazazi baada ya watoto wao kupewa adhabu ya viboko kwa kuvunja sheria za shule.
Walimu walilazimika kutoa adhabu ya viboko viwili viwili kwa wanafunzi ambao walikutwa wakishabikia ugomvi wa wanafunzi wawili waliokuwa wakigombana muda wa mapumziko ya masomo.
Wakati zoezi la kuwachapa wanafunzi hao likiendelea ndipo ghafla baadhi ya wazazi waliokuwa katika zoezi la ugawaji wa vyandarua jirani na shule hiyo baada ya kuona tukio hilo walifika shuleni hapo na kuanza kuwashambulia walimu waliokuwa wanatoa adhabu.

Hatua hiyo ya walimu kushambuliwa kwa kucharazwa viboko vimesababishwa kupatwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao huku wakionyesha kukata tamaa kufundisha kutokana na kushambuli na wazazi pindi wanapo jaribu kurudisha nidhamu kwa baadhi ya wanafunzi wanao kiuka kanuni za shule.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwabagole na baadhi ya wazazi na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wanazungumziaje tukio hilo na kusema kuwa kitendo hicho siyo kizuri kwakuwa yanaingilia utendaji wa majukumu ya walimu jambo linasababisha walimu kushindwa kufanya kazi zao kwa uhuru na kuwataka wazazi kuacha kujikulia sheria mkononi.
 Mwalimu mkuu wa shule hiyo Shilinde Nkalinga Mwenyekiti wa chama cha walimu CWT wilaya ya Kwimba Lameck Mahewa na mwakilishi wa walimu wanawake katika wilaya hiyo wameelezea kusikitishwa na kitendo hicho na kutaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya wazazi waliofanya kitendo hicho ili iwe fundisho wa wengine wenye tabia kama hizo

 Star tv imefika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kwimba Pili Mushi ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Halimashauri hiyo Pendo Malabeja wameelezea kusikishwa juu ya tukio hilo kwa kusema kuwa tayari upelelezi umeanza na hivyo wahusika watachukuliwa hatua mara moja

 Shule ya Msingi Mwabagole inajumla ya ya wanafuzi Zaidi 500 na inawalimu 12 kati yao 9 ni wanawake ili anzishwa mwaka 1937 ikiwa ni shule ya kanisa katoriki

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni