Shilole anaweza akawa anafurahia bata za Marekani baada ya kutumbuiza kwenye show nchini humo, lakini bado BASATA haijamalizana naye.
Katibu
Mtendaji wa baraza la sanaa la taifa, BASATA, Geofrey Mngereza
ameiambia Radio 5 ya Arusha kuwa adhabu aliyopewa Shilole ya kufungiwa
kutojihusisha kwenye masuala ya sanaa kwa mwaka mmoja haijafutwa.
Mngereza
alidai kuwa adhabu iliyotolewa kwa Shilole imetokana na sheria na
kanuni zilizotokana na bunge na kwamba kwa sasa wanakusanya ushahidi ili
kuchukua hatua.
0 comments:
Chapisha Maoni