Rais Kikwete Amtaja Mhusika wa Sakata la Richmond....Asema ni Yule Anayetembea na Tundu Lissu Kila Siku Kwenye Kampeni
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.
Kikwete
aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa
Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla
ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua
jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa
NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.
Kadhalika,
Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja
na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.
Suala
la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa
baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo
kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.
Kila
sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa
likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu
kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.
Mgombea
urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema
akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi
wanaosababisha umaskini nchini.
0 comments:
Chapisha Maoni