Aliyekuwa
mgombea wa kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi jimbo la mtama
SELEMANI METHEW amekihama chama hicho na kuondoka na wana CCM wapatao
704 na kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa kile
anachodai hakutendewa haki katika mchakato mzima wa kura za maoni.
METHEW
amesema kuondoka ndani ya CCM kumetokana na maamuzi ya wananchi ambao
wameona haiwezekani na haitawezekana kiongozi wanayemuitaji kufanyiwa
hila na mizengwe,kudhulumiwa haki yake ya msingi ya kuwaongoza wananchi
wa jimbo la mtama.
Amesema
jimbo la mtama halihitaji usanii bali linaitaji mgombea shupavu
atakayeweza kupambana na mgombea wa CCM Nape Nnauye huku akisisitiza
uwezo huo anao.
Mkutano huo umeudhuriwa na wanawake wengi ambao kwa sehemu kubwa ndiyo waliorudisha kadi za CCM.
Mkutano
huo ulipambwa na vimbwanga mbalimbali likiwemo tambiko rasmi
lililotumika kumzindika mgombea huyo ikiwa ni pamoja na kumpa nguvu na
kumkinga na majanga ili aweze kufanikisha kampeni na kuibuka na ushindi.
0 comments:
Chapisha Maoni