test

Alhamisi, 20 Agosti 2015

BREAKING NEWS:Ngumu kuitoa CCM madarakani baadae-Kigwangalla



Mmoja ya vijana waliokuwa wametangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.

Hamisi Kigwangalla ambaye hakuweza kufanikiwa kufikia tano bora, amefunguka na kusema kuwa itakuwa ngumu sana kuking'oa CCM madarakani huko mbele kuliko ilivyo leo.
Akipiga stori leo katika kipengele cha Kikaangoni cha kuchat katika ukurasa wa facebook wa EATV Dk. Kigwangalla amesema kuwa itakuwa vigumu kwa chama tawala CCM kutoka madarakani kwa baadae kuliko wakati huu wa sasa.
Dk. Kigwangalla aliandika maneno hayo baada ya moja wachangiaji kuweka baadhi ya kashfa ambazo zimefanyika chini ya uongozi wa CCM katika awamu mbalimbali na kuonyesha jinsi gani chama hicho kimeuwa mfumo wa uchumi na kuharibu mambo mbalimbali, ndipo hapo Kigwangalla alipoandika kuwa itakuwa ngumu kuiondoa CCM madarakani kwa baadae kuliko wakati wa sasa.
"Nakushukuru kwa kubaini hayo. Ingekuwa kwenye nyumba za dini ningeuliza...ni nani aliye msafi hata akamnyooshea kidole mwenzie? Mengi ya hayo maskendo unayoyasema yalitekelezwa na baadhi ya viongozi ambao leo hii wamepokelewa UKAWA kama malaika...na hata waliowapokea, japokuwa bado hawajapata dola, wanashare ya kutosha ya maovu yao...hivi ni lini walijibu ama kujisafisha dhidi ya tuhuma kedekede zilizowahi kuletwa kwao? Suluhu haiwezi kuwa kuiondoa CCM kwa kutumia wana CCM waliokataliwa na kutapikwa na mfumo wa CCM iliyo kwenye harakati za kufanya mabadiliko, Nikuhakikishie tu jambo moja kwamba, CCM itashinda uchaguzi wa mwaka huu, na ikishinda itaendelea na harakati za mabadiliko, itazaliwa upya na itakuwa jambo gumu zaidi kuing'oa madarakani huko mbele kuliko leo," aliandika Dk. Kigwangalla.
Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla amesema kuwa anachukizwa na kitendo cha chama chake cha CCM kulea watu ambao ni wachafu ndani ya mfumo CCM na Serikali yake jambo ambalo linafanya wajilimbikizie mali.
"Sipendi watu wachafu wanavyolelewa kwa muda mrefu ndani na mfumo wa CCM na serikali yake. Ona sasa CCM ilivyomlea Lowassa, amejilimbikizia mali na mpaka leo ana uwezo wa kuhonga kila mtu ili mradi tu apate Urais..." Dk. Kigwangalla aliandika hivyo huku akimtuhumu Lowassa.
KUKATWA JINA
Dk. Hamisi Kingwangalla alisema kuwa aliumia sana baada ya jina lake kuona halipo katika tano bora kwani alikuwa anaamini kuwa siasa zilipofikia sasa na zama tulizopo alihitajika mwanamabadiliko na mwanamapinduzi mwenye sura ya ujana, hivyo alipoona amekatwa alisononeka ila amedai kuwa alipoona jembe limepita anaamini kuwa baada ya Oktoba utendaji wa Serikali utabadilika.
"Niliumia roho baada ya kukuta jina langu halimo kwenye tano bora, maana nilitarajia kuwa kwa siasa zilipofikia na kwa zama tulizopo alihitajika mwanamabadiliko na mwanamapinduzi mwenye sura ya ujana kama yangu, lakini cha kujipa matumaini ni kwamba, tumepata jembe la uhakika, mtu muadilifu, msafi na mchapakazi. Tingatinga ambalo lina bidii na kazi na nina hakika baada ya Oktoba utendaji serikalini utabadilika sana," aliandika Dk. Kigwangalla
Kwa upande mwingine ameuponda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa ni watu walipoteza dira na wamemomonyoka kimaadili na kusema kuwa wameondoka katika heshima ya kuwa wapinzani wa kweli na sasa wamekuwa CCM B.
"UKAWA wamepoteza dira, wamemomonyoka kimaadili , hawana wanaloamini, wameondoka kwenye heshima ya kuwa wapinzani wa kweli, wamegeuka CCM B, hawana jipya, wana mgombea wa ndani ya status quo, asiye na chembe ya mabadiliko ndani yake....wamepoteza uhalali wa kisiasa na hawapaswi kuaminiwa hata kidogo...maana kwa miaka zaidi ya minane walikesha wakimchafua Lowassa na wakapata umaarufu na heshima kubwa kwa kutaja mchwa wanalimomonyoa Taifa kwa ufisadi na mkubwa wao akiwa Lowassa, leo wamemeza matapishi yao bila aibu!" Aliandika hivyo Dk. Kigwangalla.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni