Lile sakata la mrembo Wema Sepetu kutakwa kimapenzi na mpenzi wa msanii mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Nuh Mziwanda limeendelea kushika kasi ambapo Wema ameibuka na kuwavua nguo kwa kuwatolea maneno ya shombo.
Wema alitoa maneno hayo hivi karibuni
baada ya Shilole na Nuh kumgeuka na kusema kwamba aliwachezea mchezo
mchafu ili kuwagombanisha kwa sababu anawaona wanapendana hivyo
alimtafuta mtu ambaye anaendana na sauti ya Nuh ili tu amharibie.
“Sijui kwa nini Wema kanifanyia hivi
najua anataka tu kunigombanisha na mpenzi wangu kwa sababu hata
ukisikiliza hiyo rekodi utasikia sauti ya Mirror akizungumza, hapo ndiyo
ujue kuna mchezo mchafu sana na kwa hilo amefanikiwa lakini sisi huku
mapenzi yetu yanaendelea,” alisema Nuh.
Kutokana na maneno hayo Wema alicharuka
na kusema kwamba hawezi kutoa rekodi ya uongo na kumsingizia Nuh kwani
ni mpuuzi na hawezi kujilinganisha naye kutokana na kwamba ni staa
mkubwa.
“Nuh alinipigia na kunitaka kimapenzi
ndipo nikaamua kumrekodi na hiyo ni sauti yake haijatengenezwa kama wao
wanavyodai, kwanza nawashangaa hivi ningetengeneza sauti feki ili iweje,
Nuh na Shilole siyo levo yangu ni wasanii wachanga sana, mimi ni staa
mkubwa Tanzania na hakuna wa kulinganishwa na mimi labda nje ya Bongo.
"Nitafute kiki kwa kina Shilole na Nuh kweli? Si bora nitengeneze kiki
kwa kina Davido na wasanii wengine wakubwa duniani, hao si levo yangu
jamani,” alisema Wema kwa sauti ya hasira.
Kabla ya kupatana, Nuh na Shilole
waligombana hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni
baada ya mrembo huyo kupokea sauti hiyo iliyosikika Nuh akimtongoza
Wema.
0 comments:
Chapisha Maoni