Jiji
la Dar es Salaam limepiga marufu maandamno yeyote ya vyama vya siasa
hasa wakati wa kampeni na kwamba kufanya hivyo ni kinyume na sheria na
hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa chama au wafuasi wowote
watakaobainika kufanya maandamo hayo.
Agizo hilo kali kwa wafuasi na vyama vya siasa imekuja siku moja tu
kabla ya kuanza kampeni za uchaguzi mkuu, ambapo kwa mujibu wa mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam vyama vyote vya siasa na wafuasi wao watakaofanya
kampeni zao Dar es Salaam hawanabudi kuachana na dhana ya maandamo
kuelekea kwenye viwanja vya mikutano kwani hatua kali zitachukuliwa
dhidi yao.
Kwa upande wa jeshi la polisi wanasema wako imara katika kutekeleza
agizo hilo na kwamba hawatovumilia chama au kikundi chochote kitakacho
sababisha uvunjaji wa amani katika kipindi cha kampeni.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amewataka
watendaji katika mitaa kutokukubali watu watakaokufa kwa kipindupindu
kuzikwa na ndugu zao kwani inaweza kuwa chanzo cha kuzidi kusambaza
ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa maafisa wa afya wanasema ugonjwa huu wa kipindupindu
wakati wa kiangaza husambaa haraka zaidi, huku ulaji vyakula vilivyopoa,
kutokunawa mikono vizuri, ulaji hovyo wa matunda vikitajwa kuwa moja
ya sababu za ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyoitoa kwa waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam mpaka sasa kunawagonjwa 36 wa kipindupindu huku wagonjwa
wapya wakiwa 9 ambapo kata zilizo athirika zaidi zikiwa ni Mwananyamala,
Manzese, Saranga, Kimara, Ubungo,Kigogo, Tandale na Kijitonyamalas.
0 comments:
Chapisha Maoni