vyama kusema havijawahi kukaa na kukubaliana juu ya suala hilo hilo.
Taarifa kutoka Shinyanga zinasema tatizo kubwa linaonekana ni CHADEMA kung’ang’ania kusimamisha mgombea wake katika kila nafasi kuanzia ubunge hadi udiwani.
Katika nafasi za ubunge kwenye majimbo matatu yaliyopo wilayani humo, UKAWA walitaka vyama vitatu vya CHADEMA, CUF na NCCR visimamishe mgombea wake, lakini CHADEMA waligoma kwa kigezo cha kudai wao ndio wanaokubalika zaidi.
Hatua hiyo imesababisha Chama cha Wananchi (CUF) kutoa tamko kuwa umoja huo haupo Mjini Kahama kwenye suala la kusimamisha mgombea mmoja, kwa sababu CHADEMA waligoma makubaliano ya kuachiana kata na majimbo ya ubunge.
Kwa sasa vyama vya NCCR-Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na NLD vimekubaliana kufanya kampeni za pamoja, ili kuwanadi wagombea wao waliosimamishwa kwenye nafasi za udiwani na ubunge katika Wilaya ya Kahama, lakini hawatakuwa na ushirikiano wowote na CHADEMA
0 comments:
Chapisha Maoni