test

Alhamisi, 27 Agosti 2015

MAGUFULI: Nitaunda serikali yenye mawaziri wenye Nidhamu



 
Mgombea Urais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dakta JOHN MAGUFULI amesema iwapo atapata ridhaa ya wananchi ya kuingoza Tanzania
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Sumbawaga mjini mkoani Rukwa,ndani ya Uwanja wa Nelson Mandela kwenye mkutano wa kampeni,pichani nyuma ni Waziri Mkuu Pinda akishuhudia tukio hilo
Mgombea Urais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dakta JOHN MAGUFULI amesema iwapo atapata ridhaa ya wananchi ya kuingoza Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao ataunda serikali yenye mawaziri watakao kuwa na nidhamu na kuwataka kuwatumikia wananchi hususan wakada ya chini. 
Dakta MAGUFULI amesema hayo mjini SUMBAWANGA mkoani RUKWA wakati wa mkutano wake wa kampeni wa kuomba kura kwa wakazi wa mkoa huo.    
Akinadi sera ya Chama cha Mapinduzi kwa wananchi wa mji wa SUMBAWANGA, Dakta MAGUFULI amewahakikishia wananchi hao kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuongoza nchi ataunda serikali itakayozingatia nidhamu na uwajibikaji kwa lengo la kuendeleza imani kwa wananchi na hivyo CCM kuendelea kuongoza dola
Dakta MAGUFULI amewaahidi wakazi wa SUMBAWANGA kuwa mbali na kumpigia kura ya ndio yeye binafsi pia amewaomba kuchagua viongozi wa ngazi ya Ubunge na Udiwani toka CCM ili aweze kuwaagiza na kutekeleza yale yote waliyoahidi kwa lengo la kuwatatulia kero mbalimbali wananchi wa Tanzania  
Kwa upande wake Mbunge wa zamani wa jimbo la KWELA CRISTIANI  MZINDAKAYA na Waziri Mkuu MIZENGO PINDA wa kawathibitishia wananchi hao kuwa Dakta MAGUFULI ni chaguo sahihi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni