SIKU chache baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Kawawa kushindwa katika kura za maoni ya ubunge ndani ya CCM katika Jimbo la Liwale mkoani Lindi, kaka yake, Vita Kawawa naye ameripotiwa kuanguka katika kura za maoni jimboni Namtumbo, Ruvuma.
Vita
(51) aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 2005, amezidiwa nguvu
na washindani wake, Edwin Ngonyani aliyeongoza kwa kupata 12,606 na
Salome Sijaona aliyeshika nafasi ya pili kutokana na kura 7,002.
Kwa
mujibu wa Juma Mpeli, Katibu wa CCM Songea Mjini aliyesimamia kura hizo
kutokana na Katibu wa Namtumbo, Aziz Fakir kwenda kuwania ubunge Songea
Mjini, Vita amepata kura 2,749 na hivyo kushika nafasi ya tatu.
Mpeli
alisema uchaguzi huo ulikuwa marudio, baada ya ule wa awali uliompa
ushindi mbunge huyo kuonekana kuwa na hitilafu. Wengine na kura zao
baada ya marudio ya kura ni Fintan Kilowoko (1,959), Mussa Chowo
(1,229), Mwenyeheri Ndimbo (939) na Ally Mbawala (452).
Mbali
ya Vita, madiwani 18 pia wameripotiwa kuanguka katika kura za maoni,
akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo,
Steven Nana.
Nako
katika Jimbo la Tunduru Vijijini ambako pia kulikuwa na hitilafu katika
kura za maoni, mbunge wa jimbo hilo, Ramo Makani ameibuka mshindi.
0 comments:
Chapisha Maoni