Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba amesafiri kutoka jijini Dar es Salaam hadi nchini Burundi kwa shughuli ambazo hazijafahamika wazi.
Profesa
Lipumba aliondoka Dar es Salaam, Alhamisi ya Agosti 6 mwaka huu
kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air), huku
ikiwa haijulikani alikoelekea muda mfupi baada ya kutangaza
kujiuzulu wadhifa wake wa uenyekiti wa CUF, kwa kile alichodai
kutoaminiwa na wenzake ndani ya chama pamoja na kutofautiana
mtazamo na msimamo na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA).
Uchunguzi
uliofanywa na mtandao huu tangu kuondoka nchini kwa Profesa
Lipumba, umeonyesha kuwapo kwa upotoshaji wa makusudi wa mahali
aliko sasa,na kwamba hata kabla ya kuondoka, kulikuwa na
jitihada kubwa za kuficha mwelekeo wa safari yake.
Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) Dar
ambapo Lipumba alifika saa saba mchana siku ya alhamisi na
kuonwa na baadhi ya watu waliohojiwa na mtandao huu,alifika
eneo hilo akiwa amevaa suti ya rangi ya bluu iliyokoza na
shati jeupe.
Baadhi
ya watu wake wa karibu waliohojiwa kuhusu safari yake
hiyo,walieleza kuwa alipanga kusafiri kwa ndege ya shirika la
Kenya (Kenya Airways-KQ 485),lakini mashuhuda waliokuwa uwanja wa
ndege walieleza kuwa hakusafiri na ndege hiyo.
Mashuhuda
hao walieleza kuwa Profesa Lipumba alifika uwanjani hapo akiwa
na walinzi wawili na akiwa mwingi wa wasiwasi,huku macho yake
yakiwa yameiva kwa wekundu, na aliondoka na ndege ya Rwanda
Air saa tisa alasiri.
Taarifa
zilizopatikana muda mfupi baada ya kuondoka,zilieleza kuwa
alitua Rwanda na baadaye aliruka tena kuelekea Uswisi.Lakini
baadaye ilidaiwa kuwa alisalia nchini Rwanda huku ikiwa
haijulikani shughuli aliyokuwa akiifanya.
Baadhi
ya wanachama wa CUF waliozungumzia kuondoka kwake,walihoji
namna safari hiyo ilivyoandaliwa,huku wakihusisha kuwa na
msukumo wa wanasiasa wenye nguvu hapa nchini.
Hata
hivyo, mtandao huu jana ulithibitishiwa na mmoja wa wanasiasa
wenye mtandao mpana wa mawasiliano ndani na nje ya nchi kuwa
Profesa Lipumba baada ya kutua uwanja wa ndege wa
Rwanda,alisafiri kwa njia ya barabara kuelekea Burundi, ambako
hata hivyo haijulikani yuko sehemu gani na anafanya shughuli
gani.
0 comments:
Chapisha Maoni