Kundi la muziki wa bongo flava nchini, Yamoto Band wanatarajia kukwea
pipa kwenda Afrika Kusini kwa ajili yakufanya video ya wimbo wao ‘Cheza
kwa Madoido’ na muongozaji mahili barani Afrika, Godfather.
Yamoto Band ambao usiku wa kuamkia jana walitwaa tuzo ya Kili katika
kipengele cha ‘Kikundi bora cha muziki (Bongo Flava) wameamua kwenda
Afrika Kusini kufanya video ikiwa ni hatua za awali za kuingia katika
soko la kimataifa.
Aidha Yamoto Band wameachia video ya wimbo wao mpya unaoitwa
‘Nisambazie Raha’ unaofanya vizuri sana katika vituo vya radio
iliyofanyika chini ya uongozaji wake Isangi Mental.
0 comments:
Chapisha Maoni