Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) ameshinda kesi aliyomfungulia aliyewahi kuwa mchumba wake Faiza Ally ambaye pia ni mama wa mtoto wake wa kike aitwaye Sasha.
Kwa mujibu wa maelezo ya Faiza kupitia akaunti yake ya Instagram,
mahakama imetoa hukumu ambayo ni mtoto achukuliwe na kulelewa na baba
yake mzazi.
Sugu alimshitaki Faiza kwa madai kuwa hana maadili na ana hofia kuwa
atamharibu mtoto wao, hivyo alitaka kumchukua mtoto kutoka kwa mama yake
aishi naye.
Hiki ndicho amekiandika Faiza baada ya hukumu kutolewa:
“Sielewi
Joseph ameshindaje kesi- ushahidi wa picha peke yake sioni kama
unatosha mimi kupokonywa mtoto wangu,mtoto wangu ni mdogo sana
ananihitaji sana, na sita rudi hata ikibidi kuuza kila nilicho nacho kwa
ajili ya kusimamia hili.
"Sijapewa nafasi nimepelekwa mahakamani ijumaa na leo jumanne nimepewa hukumu/ mwanangu achukuliwe….. hapana ! sitarudi nyuma na haitakua rahisi ninakata rufaa na kutafuta wakili wa kunisimamia hili.
"Mwanangu anasoma vizuri anaishi vizuri na naamini kwenye mikono yangu yuko salama zaidi ya kokote/ yaani kuhusu kukosa kukaa na mwanangu ni bora kufa kuliko kuishi nikimuona sasha ana lelewa na mama mwingine ikiwa mimi mama yake niko hai na makini katika malezi ya mtoto wangu.
"Nina ndoto na mwanangu nyingi sana , nahitaji kuishi nae yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu/ nampenda sana mwanangu na sijashindwa kumlea.
"Naona uchungu sana kupelekwa mahakamani na kupokonywa mtoto wangu bila sababu za msingi .
"Sitaogopa cheo chake cha ubunge kamwe ntasimama kama mama mwenye haki kwa mtoto wake …mungu naomba nielekeze.nisimamie na unihukumie huu ukatili ninao fanyiwa na baba sasha …..”

0 comments:
Chapisha Maoni