KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ameanza vibaya ziara yake
wilayani Sengrema, Mwanza baada ya wananchi kumzomea.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana alilazimika kumshusha jukwaani na kisha aliwaomba radhi wananchi hao.
Tukio hilo limetokea leo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Zeno uliyopo Sengerema mjini, Mwanza.
Katika mkutano huo, Nape alizungumza maneno yaliyowatibuwa wananchi hasa wale wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa UKAWA.
Kwenye kauli zake Nape ambaye yupo katika
ziara moja na Kinana aliwaambia wananchi hao kuwa, baadhi ya vijana
wamekuwa wakipewa viroba ili wafanye fujo.
Nape aliwalaumu vijana hao kwamba,
wanapewa pombe aina ya viroba na viongozi wa vyama vya upinzania ili
kwenda kufanya fujo katika mikutano ya chama hicho tawala.
“Chadema kimechoka sasa hivi lakini nyie
vijana bado mmeng’ang’ani tu, mnapewa viroba na vikisha panda
mnashikilia bendera ya ‘Peoples Power’ bila kufahamu kwamba, chama chenu
kimeisha poteza mwelekeo.
“Kuna watu wanasema eti CCM ifungashe
vilago vyake katika Wilaya ya Sengerema kwa kuwa Chadema inaingia katika
uchaguzi huu, hicho kitu hakitawezekana na wao ndio wataondoka,
mtang’ang’ania sana,” amesema Nnauye.
Kauli hiyo iliyosababisha baadhi ya wafuasi wa Chadema kuanza kuzomea na hata kusababisha mkutano huo kusimama kwa saa moja.
Hata hivyo, Kinana hakuweza kuvumilia
hali hiyo na kuamka kutoka sehemu aliyokuwa amekaa na kumfuata Nape
kumwambia ashuke kutoka jukwaani na kutumia nafasi hiyo kuwaomba radhi
wananchi hao.
Katika hatua hiyo, Kinana alitumia nafasi
hiyo kuwaweka sawa wananchi hao kuwa CCM ipo imara na haitetereke kwa
chochote na kwamba, itatumia kanuni na misingi ya chama hicho katika
kuijenga nchi na kuleta maendeleo.
0 comments:
Chapisha Maoni