test

Jumanne, 9 Juni 2015

Siwema adaiwa kujirudi kwa Nay wa Mitego>>>>




Mzazi mwenzake mwanamuziki nchini Tanzania, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Siwema, anadaiwa kuanza kurudisha majeshi kwa mzazi mwenzake baada ya kutengana na kunyang’anywa mtoto.
 
Inadaiwa kuwa sambamba na maneno machafu aliyotoa mwanadada huyo kwa mwanamuziki Nay, ameonesha kujishusha baada ya mambo yake kwenda ndivyo sivyo baada ya kutengana kwao.
 
Inadaiwa kuwa ndugu wamekuwa wakimsumbua Nay, kwa kumpigia simu kumuombea msamaha ndugu yao kutokana na mambo yake kuwa magumu kadri siku zinavyoeenda hususan kesi yake iliyopo mahakamani ya kujipatia mali kwa njia isiyo halali.
 
Kwa mujibu wa Nay, amekriri ndugu wa Siwema, kumsumbua katika simu na kudai kuwa hawezi kurudiana nae na kuongeza kuwa mama yake ndiye aliyekuwa mtetezi wake lakini sasa hataki hata kusikia habari zake.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni