Waziri wa maadili nchini Uganda Simon Lokodo amedai kuwa ongezeko la
maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi yanazidi kuongezeka zaidi kutokana na
waganda wengi kufanya ngono mchana badala ya kula chakula cha mchana.
Pia waziri huyo aliendelea kwa kusema kuwa inabidi wapenzi waaminiane
zaidi na kuelekeza macho yao kwenye kupunguza ngono zembe,na kuiambia
kamisheni ya kuzuia maambukizi ya Ukimwi kuelekeza nguvu zao kwenye
vyombo ovya habari ili kuwakumbusha wananchi waliosahau.
Kwa sasa nchini Uganda, kuna zaidi ya watumiaji wa dawa za kuongeza
maisha 600,000 huku asilimia 90 ya dawa hizo zinafadhiliwa na mataifa ya
nje.
0 comments:
Chapisha Maoni