******
Shindano
la Fanya Kweli Kiwanjani limefikia tamati kwa jiji la Dar es salaam
huku wapenzi wa bia ya Tusker wakishuhudia baa ya Kinondoni M.K Pub
ikiibuka kidedea baada ya kuzibwaga baa nyingine 9 zilizokuwa zinachuana
kwenye shindano hilo.
Shamrashamra
za kuipongeza baa hiyo zilipambwa na burudani ya muziki kutoka kwa ma
Dj wa redio E-fm na watangazaji wa kituo hicho waliojumuika na mameneja
wa bia ya Tusker kuipongeza baa hiyo.
Uchangamfu
wa kiwanja hicho uliongezeka zaidi mishale ya saa moja jioni baada ya
wadhamini wa shindano hilo kuanza kutoa zawadi kwa wateja wa bia ya
Tusker waliofuruka kiwanjani hapo.
Kwa
upande wake Bw. Francis Kimbona mteja wa siku zote kiwanjani hapo
alitoa pongezi kwa wadhamini wa shindano hilo kwa kuanzisha kitu chenye
lengo la kukuza zaidi mauzo ya baa mbalimbali za mitaa tunayoishi.
“Mashindano
kama haya ni muhimu kwa kukuza kipato cha hizi baa zetu na niwaombe tu
wadhamini waendelee kuonyesha mfano kwa jamii” aliongeza Bw. Kimbona.
Naye
meneja wa bia ya Tusker Bi. Sialouise Shayo hakusita kuipongeza baa
hiyo kwa kuibuka na ushindi huku akiwashukuru wateja wa bia hiyo kwa
kuonesha uzalendo pale walipoombwa kuzipigia kura baa zote 50
zilizoorodheshwa kwenye shindano hilo.
“Tumepokea
ushiriki mkubwa kutoka kwa wadau wakati wote wa shindano hili zaidi ya
vile tulivyotarajia, hivyo nitoe tu pongezi kwa wateja wote wa bia ya
Tusker walioshiriki katika kuzipigia kura baa za mitaa wanayoishi ili
kuziwezesha zishinde shindano hili.” aliongeza Bi Shayo.
Kampeni
hiyo ambayo imedumu kwa takriban muda wa wiki tano imekua na lengo la
kuziibua baa mbalimbali za mitaa tunayoishi na kuzitangaza kwa wadau wa
kinywaji cha Tusker ambapo wadau hao walipewa jukumu la kushiriki
kuzipigia kura baa zetu pendwa ili zishinde shindano hilo.
Kupitia
bia ya Tusker mameneja wa kinywaji hicho waliweza kuorodhesha baa 50
kwenye shindano hilo ambapo kwa muda wa wiki tano wa kampeni baa 10
zilipata kuchuana vikali kila wiki ili kuweza kumpata mshindi mmoja tu.
Hivyo
basi ndani ya wiki tano za shindano baa ambazo ziliibuka kidedea ni
pamoja na;- “Toroka uje ya Kimara-Korogwe, Yenu bar ya Ubungo-Maji, New
Jambo bar ya Mabibo, Kilwa road Pub ya Kurasini na “MK Pub ya Kinondoni
iliyofunga shindano hilo.
Shindano hilo limefikia tamati kwa mkoa wa Dar es salaam huku mipango ya kulisogeza mikoani pia ikiendelea kuwekwa vizuri.
Kwa taarifa Zaidi tembelea;
Kurasa za facebook Tusker Tanzania na Twitter @Tusker Tanzania
0 comments:
Chapisha Maoni