test

Jumanne, 23 Juni 2015

MWANAMUZIKI MARIAH CAREY AANGUKIA KWA BILIONEA!>>>


Nyota wa R&B, Maria Carey akiwa na bilionea, James Packer.

CANNES, Ufaransa
HISIA ni kitu kingine! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya nyota wa R&B, Maria Carey, 45, kunasa katika penzi la bilionea, James Packer, 47, raia wa Australia.Maria, aliwahi kuolewa na Nick Cannon lakini waliachana Agosti mwaka jana kwa talaka baada ya kudumu kwenye uhusiano kwa miaka sita wakiwa na watoto wawili mapacha.
Taarifa ni kwamba hivi sasa mwanamama huyo mrembo amenasa kwenye penzi la bilionea huyo kijana. Imeripotiwa kuwa, Maria na James wamekuwa karibu na wamekuwa wakionekana pamoja wakila raha huku wakionekana sehemu mbalimbali kama Casino, migahawani na kwenye boti wakiwa wameshikana mikono kimahaba.
Bilionea huyo ameripotiwa na Jarida la Forbes kuwa anashika namba nne kwa utajiri nchini Australia.
 

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni