test

Ijumaa, 12 Juni 2015

Membe: Nikikatwa Nitampigia Kampeni Profesa Mwandosya......




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kama CCM haitampitisha kuingia tano bora, atampigia kampeni kwa moyo wa dhati Profesa Mark Mwandosya iwapo ataingia fainali ya kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.
  
Membe aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama   wa CCM kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya waliojitokeza kumdhamini.
 
Alisema unapozungumzia viongozi waadilifu nchini, Profesa Mwandosya ni namba moja, kwani amekuwa kiongozi mwenye maadili ya uongozi na mwenye upendo wa dhati kwa wengine.
 
“Natamka hili kwa moyo wangu wa dhati, jina langu lisiporudi ndani ya chama, nitampigia kampeni Profesa Mwandosya. Sina tatizo lolote hata  wakisema  mimi nimuachie  Mwandosya nipo tayari, kwani ndiyo viongozi  wanaotakiwa kama yeye  kwa sasa kuongoza nchi yetu,” alisema.
 
Kauli hiyo ni ya kwanza kutolewa na mmoja wa wagombea urais kwa tiketi ya CCM. Wagombea wengi wamekuwa wakieleza kuwa wameamua kuingia kwenye mbio hizo kwa kuwa hawajaona mgombea mwenye sifa zaidi yao.
 
Wakati akitangaza nia ya kugombea urais mkoani Lindi, Membe alisema: 
 
“Nimetafakari sana kuhusu urais nimeona niombe. Nimejilinganisha na watu wengine wote wanaotia nia, na baada ya kumpitia mmoja baada ya mwingine, nimeona Lindi tuna nafasi ya kuchukua na kuwa na kiongozi wa juu Tanzania.”
 
Na baada ya kuzungumza kwa kirefu aliuhoji umati akisema, “nani kama Membe?” na kujibiwa “hakuna”.
 
Kuhusu mipango yake kwa Mkoa wa Mbeya, alisema anatarajia kuboresha huduma za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa kuwa  ni kitovu cha uchumi.
 
Awali katibu wa CCM wa mkoa, Alhaji Mwangi Kundya alisema  jumla ya wanachama 877 walijitokeza kumdhamini Membe licha ya kwamba wanaotakiwa ni 30 tu.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni