Mwanaume
mmoja aliyetambulika kwa jina la Brandon Cohen, mkazi wa mji wa Los
Angeles huko Marekani ametoa kali ya mwaka baada ya kuamua kuvaa viatu
vya kike ili kupima ni kiasi gani Wanawake wanapata maumivu wavaapo aina
ya viatu hivyo.
Brandon Cohen aliamua kutenga siku maalumu kuvaa viatu hivyo vijulikanavyo kama High heels, baada ya kusikia malalamiko kwa wanawake wengi kwamba viatu hivyo vinawaumiza.
“Nilitaka kufahamu ni kwa nini Wanawake wengi wanalalamika kwamba viatu hivi vinawaumiza, na kwa nini sasa wanavivaa?”, alisema na kuhoji Brandon Cohen.
Brandon Cohen, akikata mitaa huku akiwa amevaa viatu vya kike Brandon Cohen, siku hiyo aliavaa viatu hivyo na kuendelea na ratiba yake kama kawaida, ambapo alitoka kwenda kazini, kutembea mitaani, kuendesha gari na kwenda kwenye maduka mbalimbali ya shooping ambapo alipata changamoto ya watu wengi kumuangalia kwani ilionekana ni kitu cha ajabu kwa mwanaume kuvaa viatu vya kike.
“Changamoto nyingine niliyoipata ni kwamba kila nilipopita nilisikia minong’ono watu wakisema kwamba mimi ni shoga, kuna wakati nililazimika kuegesha gari mbali kidogo na maeneo ya maegesho ili kukwepa watu”, alisema Brandon Cohen.
Brandon Cohen, akiwa kwenye harakati za kuegesha gari lake. Brandon Cohen alisema pamoja na yote hayo lakini aligundua kwamba wanawake wanapata maumivu makali sana wavaapo mavazi hayo, lakini wanapenda kuvaa viatu hivyo sababu wanapendeza na watu watu hupenda kuona wanawake wakiwa kwenye vazi la viatu hivyo.
“Siwezi kurudia kuvaa viatu hivyo tena kwani nimeumia sana, haya maumivu ni makali sana”, alimalizia Brandon Cohen ambaye alivaa viatu hivyo kwa saa 12 tu kwani maumivu yalimzidi.

0 comments:
Chapisha Maoni