Mshambuliaji
wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo jana ameifungia timu yake ya taifa ya
Ureno magoli matatu 'hat-trick' katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Armenia kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2016).

Ronaldo alifunga magoli yake dakika ya 29, 55, 58, wakati magoli ya Armenia yalifungwa na Marcos Pizzelli 14, Hrayr Mkoyan 71 .

Ujerumani imefanya maangamizi kwa kuitanda 7-0 Gibraltar katika mechi ya kundi D ya kuwania kufuzu Euro 2016.
0 comments:
Chapisha Maoni