Balozi
wa China katika Umoja wa Mataifa, Liu Jieyi amesema kwamba suluhu ya
nguvu za kijeshi inayotaka kufanywa na Marekani dhidi ya Korea Kaskazini
haifai kupewa kipaumbele.
Liu
Jieyi amesema hayo katika kikao cha dharura cha baraza la usalama la
Umoja wa Mataifa akijibu hatua ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio
kombora lake la masafa marefu.
Hayo
yamejiri baada ya Marekani kutangaza kuwa itatumia nguvu za kijeshi
dhidi ya Korea Kaskazini ‘iwapo ni lazima’ kufuatia jaribio la kombora
la masafa marefu lilotekelezwa na taifa hilo.
Liu
Jieyi alirejelea wito wa China na Urusi kwa mazungumzo ya Korea
Kaskazini kusitisha majaribio ya makombora iwapo Marekani na Korea
Kusini zitasitisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi.
Awali
balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Nikki Haley alisema kuwa
vikwazo vya kimataifa vilivyowekewa Pyongyang kwa miaka kadhaa
havitoshi.
Amesema kuwa vitendo vya Korea Kaskazini ni ishara za kuzuka kwa mgogoro duniani.
0 comments:
Chapisha Maoni