Stori
kutoka Uingereza nimekutana nayo mtandaoni mtu wangu wa nguvu, na kama
ilivyo kawaida yangu, nafanya kushare na wewe kama hivi.
Na
stori hii inamhusu sokwe mmoja ambaye amepewa jina la Zaire, ambaye
anafugwa katika bustani moja ya wanyama London, Uingereza amesherehekea
siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 40.
Na
kama haitoshi, party yake ilikuwa poa kama ambazo huwa tumezoea kufanya
binadamu, ametengenezewa keki ya nguvu katika sherehe hiyo na moja ya
mabingwa wa kutengeneza keki za sherehe, Richard Burr.
Unaambiwa
sokwe huyu anapendelea vitu kama jelly zisizo na sukari, apples, na
karoti hivyo mwandaaji wa keki alijikuta na jukumu la kuhakikisha
anamuandalia keki itakayomfurahisha Zaire.
Hizi ni picha za Sokwe huyo akijiachia na keki akisherehekea.
0 comments:
Chapisha Maoni