MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustino Mrema ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Vunjo amekanusha kufukuzwa katika chama chake.
Alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, baada ya kuzagaa habari kuwa yeye sio Mwenyekiti wa chama
hicho.
Alisema amekuwa akishangazwa na habari zinazotolewa na kikundi cha
watu wanaojiita wanakamati wa TLP ambao wanadai kuwa yeye sio Mwenyekiti
kwani tayari wamemchagua mwenyekiti wao.
Aliongeza kuwa kama kuna mabadiliko katika chama hicho, ni lazima
yeye ajue kwani ndiye pekee mwenye mamlaka ya kufanya mabadiliko katika
chama hicho.
“Mikutano yote lazima iitishwe na mimi, hakuna mwenye mamlaka kwa
mujibu wa katiba ya chama chetu, hivyo hakuna mtu mwenye ubavu wa
kunivua uenyekiti,” alisema Mrema.
0 comments:
Chapisha Maoni