KABAAANG! Wakati supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitembea kifua mbele huku akijinasibu kuwa anasubiri kwa hamu kupata mtoto kutoka kwa mchumba wake, Zarinah Hassan ‘Zari’, imevuja picha inayomuonesha laivu mwandani wake huyo akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi ikidaiwa kuwa ni mtu wake wa nguvu, Ijumaa lina stori kamili.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Katunzi ni mtu wake Zari kitambo kabla hata Diamond hajaanzisha naye uhusiano wa kimapenzi mwishoni mwa mwaka jana na walikuwa wakikutana mara kwa mara.“Katunzi na Zari walijuana kitambo sana. Yaani suala la Zari kuibuka Bongo na kufanya mambo yao haikuwa ishu na hata Katunzi alikuwa akiibuka Sauz (Afrika Kusini anakoishi Zari) na kuwa pamoja,” kilisema chanzo hicho.
KATUNZI ALIWAKUTANISHA ZARI NA DIAMOND
Kuonesha kwamba kina ubuyu kamili, chanzo hicho kilizidi kufunguka kuwa, hata safari ambayo iliwakutanisha Zari na Diamond kwa mara ya kwanza, mrembo huyo alikuja Dar, kumfuata pedeshee Katunzi, ndipo ‘dodo lilipomdondokea’ Diamond kama kumsukuma mlevi vile.
“Kweli Diamond ana zari kama lilivyo jina la mrembo huyo mwenye asili ya Kiganda. Siku hiyo ya kwanza kabisa walipokutana, Zari alikuwa anaibuka Bongo kuitikia wito wa mtu’we Katunzi.
NDANI YA NDEGE SASA
”Diamond alichangamkia fursa, alipoona ‘dhahabu’ inaelea ndani ya ndege katika daraja la juu (business class), akaomba namba, akakubaliwa na ndipo wakaanza kupiga mapichapicha ya selfie ambayo yalivuja na Wabongo wakaanza kujiongeza kwani wakati huo tayari Diamond alikuwa ameshaachana na Wema Sepetu ‘Madam,” kilitiririka chanzo hicho.
PICHA ZAMSHTUA KATUNZI
Kwenye mazungumzo yake, chanzo hicho hakikusita kufunguka kuwa baada ya picha za Diamond na Zari kuanza kuvuja kwa mara ya kwanza, ilidaiwa kuwa zilimshtua Katunzi kiasi cha kumtumia ujumbe mfupi wa simu Zari kumuuliza ni kitu gani kilikuwa kikiendelea kati yake na mwanamuziki huyo.“Katunzi ilibidi amuulize Zari kuhusu picha hizo, Zari akamwambia hakuna kitu chochote ni urafiki wa kawaida, hata hivyo jamaa hakujali.
DIAMOND UPOOO!!
“Diamond kama aliingia katika himaya ya Zari pasipo kujua kuna watu wanamjua kitambo atakuwa amechelewa. Pedeshee Katunzi alimjua kitambo sana Zari,” kilimalizia chanzo hicho.
PICHA TOFAUTI ZANASWA
Mbali na kumwaga ubuyu huo, chanzo hicho kilivujisha picha tofauti katika dawati la Ijumaa zinazomuonesha Katunzi akiwa kwenye pozi la pamoja na Zari kuthibitisha kwamba wawili hao ni watu wanaofahamiana.
KWA NINI URAFIKI WA SIRI?
Ijumaa lilifanya uchunguzi wa kwa nini urafiki wa Zari na Katunzi ulikuwa wa siri na kubaini kuwa wawili hao hawakutaka watu wajue kwa sababu ambazo wenyewe wanazijua lakini kitu walichokuwa wanazingatia ni mpango wa ‘kula bata’.
Timu yetu ya uchunguzi imebaini pia kuwa, wawili hao wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara kupitia simu zao za mikononi, mawasiliano ambayo bado yanafanyiwa kazi ili baadaye yapakuliwe yakiwa yameiva.
KATUNZI ANASEMAJE?
Baada ya kumsaka Zari bila mafanikio, mwanahabari wetu alimvutia waya Katunzi ili kumsikia anazungumziaje ukaribu wake na Zari, alipopatikana alijibu kwa kifupi.“Zari namfahamu, kuna nini kwani?” Alihoji Katunzi. Alipoambiwa kuwa kuna picha na habari zake kuhusu Zari alikata simu na hata alipopigiwa tena hakupokea.
KUTOKA DAWATI LA IJUMAA
Kufuatia kuwepo kwa minong’ono mingi kuhusiana na ukaribu wa Zari na Katunzi, dawati la Ijumaa linaendelea kuchimba undani wa habari hii kwa kumtafuta Katunzi, Zari na Diamond ili wote wafunguke kwa kirefu
0 comments:
Chapisha Maoni