HATIMAYE
Hospitali ya African Medical Investment Ltd (AMI) maarufu kama Trauma
Center ya Masaki Dar es Salaam, imefungwa rasmi na mmiliki wa jengo
kukabidhiwa funguo zake.
Hospitali
ya AMI na ya gharama ya juu ilikuwa ikitoa matibabu kwa viongozi wa
ngazi za juu wa Serikali, wabunge , mabalozi na wafanyabishara wakubwa
wa ndani na nje ya nchi.
Kufungwa
kwa hospitali hiyo kumetokana na kushindwa kulipa kodi ya pango kwa
zaidi ya miezi 26, inayofikia zaidi ya dola za Marekani milioni 1.6,
ambazo ni zaidi ya Sh bilioni tatu.
Makabidhiano
hayo yalifanyika jana hospitalini hapo kati ya Mwakilishi wa Kampuli ya
udalali wa Mahakama ya MEM Auctioneers and General Brokers Ltd, Elieza
Mbwambwo kwa Meneja wa jengo hilo, Zurfiq Hassanar, dalali huyo wa
mahakama alisema hatua hiyo ya kuhamishwa kwa hospitali hiyo imetokana
na uamuzi wa Mahakama Kuu.
“Ninapenda
kusema leo (jana), tunakabidhi jengo na funguo zake kwa Meneja wa jengi
hili kwa niaba ya mteja wetu, wiki mbili zilizopita tulikamata mali
baada ya AMI kushindwa kulipa deni kama ilivyoamriwa na mahakama.
“Mahakama
Kuu ilichoamuru mali za AMI zikamatwe na kupigwa mnada ili kuweza
kulipa deni lao la pango na kisha kuondolewa kwenye jengo na kumkabidhi
mmiliki wake Navtej Singh Bains,” alisema Mbwambo.
Mali
zilizokamatwa ni magari matatu ya kubebea wagonjwa (Ambulance), vitanda
maalumu vya kulaza na kuwahudumia wagonjwa, gari ndogo aina ya Mark II,
mashine mbalimbali pamoja na samahani zilizokuwa zikitumiwa katika
jengo hilo.
“Tulipokuja
awali tulitoa taarifa kwa ndugu wa wagonjwa wawe wamewaondoa wagonjwa
wao na sasa jengo ni nyeupe halina mtu ndani, hata mali tilizokamata
tutazipiga manda ingawa tunajua haziwezi kufikia thamani ya fedha
zinazodaiwa, maana kwa sasa kuna maombi mengi ya watu wanataka kufungua
hospitali hapa,” alisema
Alisema
mashine za CT -Scan, X-ray ni miongoni mwa zitakazopigwa manda huku
atakayepanga katika jengi hilo akipewa kipaumbele cha kwanza.
Hatua
hii ya kufukuzwa kwenye jengo imefikiwa baada ya mabishano ya muda
mrefu ya kisheria baina ya AMI na mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki
wa jengo hilo, Navtej Singh Bains.
Taarifa
zaidi inasema kwamba akaunti za Benki za Hospitali hiyo ya AMI katika
Benki ya EXIM zilizoambatanishwa na Mahakama zilikutwa zikiwa zimefungwa
na fedha zote zikiwa zimetolewa.
Amri ya kufurushwa kwa AMI ilitolewa Mei 7, mwaka huu na kusainiwa na Makamu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa AMI Plc, Theunis Peter Botha, ambaye pia ni Mkurugenzi
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya AMI Tanzania, aliwasilisha ombi
Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa imefilisika.
Akizungumza
kwa niaba ya wafanyakazi wenzake hospitalini hapo, Rose Sesoa, alisema
pamoja na kufungwa kwa hospitali hiyo hivi sasa hawajui hatima yao.
“Tunaiomba
Serikali ichukue hatua sasa.Wakija wawekezaji wageni wawabane kwa
maswali maana leo hili limetokea na hapa tupo Staff zaidi ya 100 hatujui
tufanye nini. Kikubwa ni makato ya NSSF ambayo imekuwa ikituma watu
wake lakini wakifika hapa wanapewa bahasha na kunyamaza huku Makato
hayapelekwi,” alisema Sesoa.
AMI
Tanzania inamilikiwa na Kampuni mama ya AMI Plc ya London ambayo
iliondolewa kwenye Soko la Hisa la London mnamo Februari 2014 baada ya
jaribio la kuuza mali zake zilizopo nchini Maputo bila kibali kutoka kwa
wanahisa.
Pia
kumbukumbu zinazoonyesha kuwa Lancet Laboratory (T) Ltd iliwasilisha
ombi la dharura dhidi ya kufungiwa kwa Hospitali ya AMI ikiwa inaidai
hospitali hiyo zaidi ya Sh milioni 150.
Hata
hivyo wakati inafungwa hospitali hiyo, baadhi ya wazabuni walikuwa
hospitalini hapo huku wakiwa hajui la kufanya juu ya hatima ya malipo
yao.
0 comments:
Chapisha Maoni