test

Jumatatu, 11 Mei 2015

Diamond Platinumz Katika Hili Umekosea,Umekosa Busara ni vyema Ukajifunza Kuweka Akiba ya Maneno



 
Nime yaandika haya baada ya kuona post ya
Diamond akikosoa vikali tunzo za kill hadi amepitiliza na kuandika yasiyo tarajiwa pengine alikuwa na hasira sana lakini tusisahau kuwa hasira haijengi!
Kwangu mimi naona amekosea sana!

Hakuna busara iliyo kuu kama ku kaa kimya! Hapa ndio naamini wasanii wana hitaji washauri wa karibu kabla ya kuandika au kusema chochote!

Diamond umekosea sana tena sana..ulikuwa na nafasi ya kukaa kimya kuonesha busara kuu!Kuna mtu alisema ukitaka kutambua mtu mwenye busara subiri akiwa na furaha sana au akiwa na hasira sana!

Naanimi Diamond hukufikiri mara mbili kabla ya kupost uliyo yapost! Kila mtu anajua wazi kuwa hizi tunzo hazijakamilika na haziwezi kukamilika kamwe na hata kama kuna mtu atapewa kuziendesha kamwe haziwezi kuwa satisfy watu wote na wakati wote!

Pengine ni kweli anayo jaribu kutuambia Diamond lakini ninacho jiuliza hii ndio busara yako ya mwisho?
Kila mdau wa muziki anajua fika kuwa hakuna mwaka ambao umekuwa na hit song nyingi kama mwaka jana na mimi nilijua utaleta malalamiko mengi sana lakini niliamini kuwa busara ndio itatumika zaidi kuliko hasira au meneno ya kuwa vunja moyo waandaji waonekane hawajafanya lolote kwa kuwa tulio wategemea hawapo!

Diamond una sahau kuwa wakati unapewa tunzo wewe kuna watu wali lalamika kuwa umependelewa na wengine wakajitoa na wengine wakatumia busara na kukaa kimya!

Jamani kama maneno ya namna hii yangekuwa yana andikwa basi yangetoka kwa Bell 9 ambaye watu walikuwa wanaamini kuwa ana stahili tunzo kila leo..lakini kijana wa watu amekuwa ni mwwnye hekima sana na nina mpongeza kwa hilo!

Diamond kusema kuwa hata usipopewa tunzo huwezi kushuka ni kuwakosea heshima Kill na Basata kwani hizi ni tuhumu zisizo na msingi kutoka kwa msanii mkubwa kama wewe ...ni kweli wana lengo la kukushusha?
Diamond umekosa busara kabisa kabisa ulipaswa kukaa kimya maana ni wachache wataamini una watetea hao ulio wataja!

Diamond jifunze kuvumilia na si kila kitu cha kukifanya public..Diamond ina maana kusema kwako hukuhangaika kuwambia watu jinsi ya kupiga kura maana hukupendezwa ina maana umegomea tunzo? Ni kweli Kill na Basata wamekuwa wabaya kiasi hiki hadi una diriki kuuliza kama wanau au kukuza muziki?

Diamond umenishangaza sana tena sana lakini na kukumbusha ujifunze kuweka akiba ya maneno na ndio busara iliyo kuu kuliko kuongea!

Diamond umeshindwa kujiuliza kwanini wengine wame nyamaza?

Mimi naamini hizi tunzo ni nzuri na ni msaada kwa wasanii pia si tunzo zilizo kamilika na hakuna tunzo zilizo kamilika duniani!

Uzuri wasanii huwa mnapewa semina kwa hiyo mnaweza kusema huko huko malalamiko yenu lakini kuongea kwenye media tena kwa njia uliyo tumia itachukuliwa ni kutaka watu wagomee tunzo hizi!

Wasanii ni vyema mkawa mnaweka akiba ya maneno ili msiwa katishe tamaa walio jitoa kuikwamua tasnia hii kwani nao hawaja kamilika!
 

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni