Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Mwenyekiti wa Mashindano,
Hussein Nyika, umesema kuwa umekata rufaa TFF kulalamikia mchezaji
mmoja wa Mbeya City kuzidi Uwanjani.
Nyika ameeleza kuwa wametuma malalamiko hayo kufuatia
mchezaji wa Mbeya City kuonekana Uwanjani wakiwa 11 badala ya 10 wakati
mmoja wao alikuwa ameshapewa kadi nyekundu.
Yanga wamefikia hatua ya kufanya hivyo baada ya beki wa
Mbeya City, Ramadhan Malima kupewa kadi nyekundu, na kisha baadaye
kuonekana tena Uwanjani wakati zikiwa zimebakia dakika takribani 6
mchezo kumalizika.
Wakati mechi hiyo ikielekea mwisho, Kocha Msaidizi wa
Yanga, Shadrack Nsajigwa, alionekana akibishana na Kamisaa wa mchezo
huo, kuhoji kwanini Mbeya City wapo 11 badala ya 10.
Nsanjigwa alionekana akiwa amepandisha munkari akitaka
kujua kipi kilichosababisha mpaka aendelee kusalia Uwanjani wakati
kanuni haziruhusu.
Mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya,
ilimalizika kwa sare ya 1-1, Yanga wakifunga kupitia Rafael Daud na
Mbeya City kupitia Iddy Naddo.

0 comments:
Chapisha Maoni