Serikali
ya awamu tano kupitia Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa
mwezi mmoja kwa mameneja wote wa mikoa wa Shirika la Umeme nchini
Tanesco kuwaunganishia umeme wananchi ambao tayari washalipia huduma
hiyo na meneja atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo ajiuzulu kazi mara
moja.
Dkt.
Kalemani ametoa agizo hilo wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya
kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini (REA),
awamu ya tatu katika maeneo mbalimbali wilayani kyela na kusema wananchi
wamekuwa wanaolipia huduma ya kuunganishiwa umeme wamekuwa wakipatia
kero nyingi bila ya kupewa huduma hiyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Hunter
Mwakifuna ameishukuru Wizara ya Nishati kuwa kuwaelekeza wakandarasi
wanaosambaza umeme vijijini kuwashirikisha viongozi wa maeneo husika,
hatua ambayo imepunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.


0 comments:
Chapisha Maoni