Wasanii
mbalimbali wa filamu na wa bongo fleva, wamekutana katika viwanja vya
Leaders Club usiku huu ili kujadiliana kuhusu utaratibu wa mazishi ya
msanii anayepamba video za muziki (video queen), Agness Gerald maarufu
Masogange.
Steve
Nyerere amesema kuwa, Masogange anatarajiwa kuzikwa Mbeya na kuwa mwili
utasafirishwa Jumapili wiki hii na kuzikwa Jumatatu.
Miongoni
mwa wasanii waliofika Leaders leo ni pamoja na Chopa wa Mchopanga,
Irene Uwoya aliyeambatana na mume wake, Dogo Janja na aliyekuwa
mtangazaji wa Clouds Media Group, Zamaradi Mketema.
Kamati ya awali iliyoundwa, imemchangua Mchopanga kuwa katibu na Zamaradi kukusanya michango.
“Lakini
tukipata taarifa kutoka kwa ndugu tutajua msiba utagharimu shilingi
ngapi kwa sasa mahitaji makubwa ni mabasi mawili kwa ajili ya
kusafirisha mwili, maturubai, vyakula na maji,” amesema Nyerere.

0 comments:
Chapisha Maoni