Wakili
Albert Msando ataongoza kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mhe. Paul Makonda kwa ajili ya kushughulikia kesi zote na
changamoto zilizojitokeza katika zoezi la kutafuta haki za watoto
waliotelekezwa na wazazi wao.
Zoezi
hilo lilifungwa hapo jana April 27, 2018 ambapo wananchi 17,000
walijitokeza, kati yao 7,184 walisikilizwa, huku 270 wakipimwa DNA.
RC
Makonda ameunda Kamati ya Wataalamu 15 wakiwemo Wanasheria, Maafisa
Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi Dawati la jinsia na Asasi za kiraia
itakayofanya kazi ya kupitia mapungufu ya kisheria na Changamoto
zilizojitokeza.
Kamati
hiyo ambayo itaanza kazi rasmi May 05, 2018 chini ya Wakili Albert
Msando ambaye ndiye Mwenyekiti wake itatoa mapendekezo kwaajili ya
kufikishwa kwa mamlaka husika ili kufanyiwa maboresho.
Utakumbuka
December 20, 2017 Wakili Albert Msando aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli katika tume itakayokuwa na
jukumu la kufuatilia mali za Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kabla
ya kuteuliwa na Rais Magufuli, September 26, 2017 Wakili Msando
aliteuliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.
Harrion Mwakyembe kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki
za kazi za wasanii.
0 comments:
Chapisha Maoni