Rais
John Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Wakala wa Umeme Vijijini
(Rea) kuondoa changamoto za kawaunganishia nishati hiyo wananchi.
Pia,
amewaagiza wakuu wa taasisi mbalimbali za umma kufanya kazi kwa
ushirikiano ili kuepuka gharama wanazoisababishia Serikali na
kuchelewesha maendeleo kwa wananchi.
Hayo
ameyasema leo Jumatatu Aprili 3, 2018 wakati akizindua kituo cha kufua
umeme cha Kinyerezi II 240MV CCPP jijini Dar es Salaam.
Rais
Magufuli amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu
gharama za kuunganishiwa umeme hivyo hatua za haraka zinahitajika
kuchukuliwa.
"Wizara
ya Nishati na Rea hakikisheni mnaongeza kasi ya kuunganishiwa umeme,
yapo malalamiko machache machache ya wafanyakazi kuomba rushwa,
yashughulikiwe hayo," amesema Rais Magufuli
Kuhusu malalamiko ya taasisi kucheleweshewa baadhi ya huduma amesema hilo linamkera na hataki kulisikia tena.
Amesema taasisi za Serikali zinatakiwa kufanya kazi kwa karibu hasa tunapotekeleza miradi mikubwa ya Taifa, tusicheleweshane.
"Mawaziri,
wakurugenzi, wenyeviti wa bodi msiache kuwasiliana ninyi kwa ninyi,
kama unaona unakwamishwa na taasisi nyingine, mambo kama haya nikisikia
huwa yananiudhi, lugha ya mitaani yananiboa kweli kweli. Shirikianeni
kwani mnawacheleweshea wananchi maendeleo," amesema Rais Magufuli.
Amesema
kuwa umeme wa uhakika unachagiza kutekeleza Tanzania ya Viwanda kwani
kwa sasa mahitaji ya nchi ni megawati karibu 1,40O lakini uzalishaji
umefikia megawati 1515.3,"Bado tunahitaji umeme wa kutosha na tuongeze
uzalishaji."
0 comments:
Chapisha Maoni