Waziri
wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck
Nchemba, ametolea ufafanuzi suala lililoibuliwa na Mbunge wa Kilwa
Kusini Suleiman Bungara, kuhusu polisi kushambulia watu msikitini na
wengine kuuawa.
Akizungumza
Bungeni leo Waziri Nchemba amesema kwamba yeye kama waziri mwenye
dhamana amelisikia suala hilo na ameagiza uchunguzi ufanyike, ili kuweza
kubaini mbivu na mbichi na sheria kufuata mkondo wake.
Sambamba
na hilo Waziri Nchemba ameitaka jamii kutohusisha makosa ya uhalifu na
masuala ya dini au siasa, kwani mhalifu anapokamatwa hakamatwi kwa imani
ya dini au chama chake, bali ni kwa makosa aliyofanya.
“Nimewaelekeza
wafanye uchunguzi wa ndani ili tuweze kupata taarifa kamili na tutatoa
taarifa, na nimuombe mheshimiwa mbunge tuepuke sana kulinganisha jambo
hilo na dini, linapotokea suala la uhalifu mtu hakamatwi kwa dini yake,
anakamatwa kwa kosa alilolifanya, watu wanakamatwa kutokana na makosa
aliyofanya wala asiunganishwe kwa dini yake au chama chake”, amesema
Mwigulu Nchemba.
Hapo
jana Mbunge wa kIlwa Kusini Suleiman Bungara maarufu kwa jina la Bwege
alimtaka Waziri atolee ufafanuzi suala la polisi kuingia msikitini na
kupiga risasi, na kuchukua baadhi ya watu ambao wengine walirudi wakiwa
marehemu.
0 comments:
Chapisha Maoni