Mbunge
wa Geita vijijini, Joseph Kasheku maarufu Musukuma (CCM), ameitaka
serikali irudishe kazini watumishi wa darasa la saba iliowafukuza
vinginevyo wabunge wenye elimu ya darasa la saba pia waondolewe bungeni.
Musukuma amesema hayo bungeni Mjini Dodoma leo Ijumaa Aprili 6, alipokuwa akichangia hotuba ya ofisi ya Waziri Mkuu.
Amesema
wabunge wakishaondolewa bungeni warudishwe kwa Viti Maalumu kama ilivyo
kwa wanawake na walemavu ili wawatetee darasa la saba wenzao.
Musukuma
amesema hotuba ya Waziri Mkuu inaonyesha mwaka wa fedha uliopita
waliojiunga na darasa la saba ni milioni mbili na walioingia sekondari
ni 500,000 jambo linalomaanisha wenye elimu ya darasa la saba ni zaidi
ya asilimi 80.
“Serikali
isiposikia kilio chetu na kuwarudisha kazini watumishi hao na wabunge
wa kambi zote kuungana na kutetea watumishi hao waliofukuzwa kazi basi
tutakutana 2020,” amesema Musukuma.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )