Msanii wa Bongo Flava kwa sasa, Mimi Mars amefunguka kuhusu kurejea katika utangazaji wa TV.
Muimbaji
huyo aliyekuwa akitangaza kipindi cha Weekend Gossip kupitia TV 1
amesema mipango ya kurejea katika utangazaji ipo ila bado ni vigumu
kuweka wazi ni kipindi gani hasa.
“Mipango inafanyika kikubwa ni ku-keep up na mimi na watajua na watapata kusikia ni lini, wapi na sehemu gani,”
Katika hatua nyingine amezungumzia maisha ya muziki na yale ya utangazaji, utofauti upo wapi.
“Hamna
utofauti kwa sababu kile kipindi watu walikuwa wanakifurahia, kusema
kweli kile kipindi ndio kilinianzisha watu waweze kujua Mimi Mars ni
nani na mashabiki wangu wengi nimewapata kupitia kipindi kile hadi
nilipoingia kwenye muziki,” amesema Mim Mars katika mahojiano na Bongo5
Mimi
Mars ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Papara’ ana historia yenye
kushabiana na ile ya dada yake, Vanessa Mdee ambaye awali alikuwa
mtangazaji wa MTV Base na Choice FM kabla ya kuingia katika muziki.
0 comments:
Chapisha Maoni