Alikiba
ambaye siku ya alhamisi ya tarehe 19, April, 2018 alifunga ndoa na
binti Aminah Rikesh kutoka nchini Kenya katika mji wa Mombasa ambapo
inatarajiwa Alikiba kuirudisha sherehe hiyo nyumbani Tanzania tarehe 29.
Siku hiyo Alikiba aliweka wazi mdogo wake Abdukiba kuwa ataoa karibuni.
Hatimaye
ahadi hiyo ya Alikiba kuhusu mdogo wake imetimia kwani msanii huyo
ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ya 'Jeraha' amefunga ndoa pia
na moja ya mtu wake wa karibu na kufanikiwa kuongeza idadi ya wanawake
katika familia yao kama ambavyo mdogo wake wa kike Zabibu anavyosema
kuwa mwanzo walikuwa wawili tu yeye na mama yake lakini ameongezeka mke
wa Kiba na kudai anatarajia kuongezeka mwingine wa nne karibuni ambae
ndiye mke wa Abdukiba.
Kupitia
mtandao wa Instagram msanii H Baba ambaye ni mtu wa karibu na kina
Alikiba ameweka wazi kuwa Abdukiba leo amefunguka ndoa na kumtakia kheri
kwenye siku yake hiyo muhimu katika maisha yake.
"Hongera
sana Abdukiba kwakuchukua jiko lako Allah akulindie ndoa yako, jambo la
kheri uja na kheri zake karibu chama la waliompendeza Mungu kwani kuoa
nijambo la kheri" alisema H Baba
Alikiba
na Abdukiba wanadhaniwa kuwa huenda wanaweza kufanya sherehe ya pamoja
April 29, 2018 jijini Dar es Salaaam ili kufurahi na watu wao wa karibu
kufuatia zoezi la wao kufunga ndoa.


0 comments:
Chapisha Maoni