Mbunge
wa Momba, David Silinde (Chadema), amehoji bungeni kuhusu taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutokuwa na taarifa
za Shirika la Ndege (ATCL) na Wakala wa Barabara (Tanroads).
Akichangia
bungeni jana mjadala wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka ujao wa fedha, mbunge huyo ambaye pia
ni Naibu Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, alisema hakutarajia kuona
ripoti ya CAG ya mwaka 2016/17 ikikosa taarifa za taasisi hizo muhimu
katika kipindi hiki ambacho zinatengewa fedha nyingi.
Alisema
taarifa za fedha za taasisi hizo zilipaswa kuwamo kwenye ripoti ya CAG
ili wahoji kama wanavyofanya sasa kuhusu kutoonekana kwa matumizi ya Sh.
trilioni 1.51.
Silinde
ambaye alihoji ni sababu za ripoti za CAG kutokuwa na taarifa za
Tanroads ili wabunge waangalie barabara za Tanzania kama zinaendana na
thamani ya fedha inayotolewa.
“Sisi
kama wabunge tunatakiwa kuhoji kwanini katika ripoti ya CAG huwa hakuna
Tanroads, tunatakiwa kuhoji; je, barabara inayojengwa inalingana na
'value for money' (thamani ya fedha)?” alisema Silinde.
0 comments:
Chapisha Maoni